Jumatano, 10 Februari 2016

Mbwana Samatta ataonekana akicheza mechi uwanja huu Ubelgiji (+Pichaz)

Bado furaha ya watanzania kumuona Mbwana Samatta akicheza soka Ulaya ipo moyoni mwao, baada ya kumuona kwa mara ya kwanza akiichezea klabu yake ya KRC Genk kwa dakika 17 February katika mchezo dhidi ya Mouscron FC, huku mchezo ukimalizika kwaKRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 1-0 ugenini.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Klabu ya KRC Genk inarudi jijini Genk kucheza mchezo wake wa Ligi katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena Jumamosi ya February 13 kucheza mechi yao 26 ya Ligi dhidi ya Beveren W iliyopo nafasi ya 13 katika Ligi ikiwa na point 26 wakati KRC Genk ya Samatta ipo nafasi ya 5 ikiwa na point 38.
krc1
Huenda Mbwana Samatta akapata nafasi ya kucheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Beveren W na kuweka rekodi ya kucheza mechi yake ya pili akiwa na KRC Genk lakini pia akicheza mechi ya kwanza ya mashindano katika uwanja wa nyumbani wa KRC Genk kama mchezaji rasmi wa klabu hiyo.
Cristal_Arena_Genk
Uwanja wa Cristal Arena unaotumiwa na KRC Genk kama uwanja wa nyumbani, ulijengwa mwaka 1999, una uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 20000, unatumika kwa michezo mingi, ila kwa kiasi kikubwa mchezo wa mpira wa miguu ndio huchezwa sana, kabla ya kuanza kwa msimu wa 2008/2009 uwanja huo ulikuwa unaitwa “Fenixstadion” ila mwaka 2007 KRC Genk walisaini mkataba na kampuni ya bia ya  Alken-Maes ili kukodisha jina.
front_stadion
large_326954
timthumb
2643449
GENK, BELGIUM - AUGUST 1: A general view inside of the Fenix Stadium ahead of the Belgian Jupiler Pro League match between KRC Genk and KFC Germinal Beerschot on August 1, 2010 in genk, Belgium. (Photo by EuroFootball/Getty Images)
soke2_090404_ground_genkcristal-arena_www.soke2_.de011
11979884-500x408
Hii ilikuwa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilichezwa mwaka 2011 kati ya KRC Genk dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Cristal Arena. Hao ni mastaa wa Chelsea John Terry na Anelka

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni